Pata taarifa kuu
DR-Congo

Serikali ya DRC yatishia kujiondoa katika mazungumzo na waasi wa M 23

Mazungumzo ya amani kati ya maafisa wa serikali wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M 23 yalianza jijini Kampala Uganda siku ya Jumapili kwa kusuasua na kuzua maswali ikiwa kikao hicho kitazaa matunda.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Kinshasa inatishia kujiondoa katika mazungumzo hayo kwa kile wawakilishi wa serikali wanasema ni tuhma zisizo za msingi zinazotolewa na kundi na waasi dhidi yao katika mkutano huo.

Tofauti zilianza kuzuka katika kikao hicho baada ya mwakilishi wa kundi la waasi Francois Tuyihimbaze Rucogoza, kuituhumu serikali ya DRC  kuwabagua waasi hao kikabila na kuwaua wanajeshi wake.

Aidha, waasi hao wanaishtumu serikali ya Kinshasa kwa kuhusika na visa vya ufisadi na kushindwa kuimarisha maisha ya wakaazi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kiongozi wa ujumbe wa serikali Waziri wa Mambo ya nje Raymond Tshibanda, alikanusha tuhma hizo na badala yake kumtaka msuluhishi wa mkutano huo Waziri wa Ulinzi wa Uganda Crispus Kiyonga kuwajibu waasi hao.

Tshibanda ametishia kujiondoa katika mkutano huo  ikiwa hawatapa muda wa kutosha wa kujibu waasi hao basi huenda wakajiondoa katika mazungumzo hayo.

Waasi wa M 23 wamekuwa wakitaka kukutana na serikali ya Kinshasa ili kutatua tofauti zao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.