Pata taarifa kuu
DRC

Rais Museveni awakashifu askari wa MONUSCO

Uganda imekashifu uwepo wa walinda amani wa umoja wa mataifa Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokarsia ya Congo na kusema kuwa ni aibu kubwa askari hao wa MONUSCO kushindwa kuzuia vita nchini Congo. 

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni AFP
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika mkutano wa mataifa ya kusini mwa Afrika SADIC jana Jumamosi,nchini Tanzania, rais Yoweri Museveni amesema kuwa kuwepo kwa askari hao wa umoja wa mataifa nchini humo ni kama wanafanya utalii kutokana na wanaendelea kushuhudia machafuko na hawafanyi lolote kuyatatua.

Tarehe ishirini mwezi Novemba waasi wa M23 waliuteka mji muhimu wa Goma katika jimbo lenye utajiri wa madini la Kivu Kaskazini baada ya kudharau mashambulizi ya anga ya askari wa MONUSCO huku vikosi vya serikali vikiukimbia mji huo.

Mkutano huo umemalizika huku mapendekezo kadhaa yakitolewa ikiwa ni pamoja na wito kwa umoja wa mataifa kurekebisha mamlaka ya MONUSCO na kuwapa uhuru zaidi wa kupambana na majeshi ya waasi katika eneo hilo sambamba na kuunda jeshi ruhu litakalo pambana na waasi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.