Pata taarifa kuu
MISRI

Wakristo wasusia kura ya rasimu ya katiba nchini Misri huku maandamano yakipamba moto

Wakati maandamano ya kupinga uamuzi wa rais wa Misri Mohamed Morsi kujiongezea madaraka yakipamba moto, mipango ya kupigiwa kura kwa rasimu ya katiba mpya imeendelea nchini humo na hatua hiyo inaendelea kuzua utata na hali ya hofu kama rais kama rais Morsi hatabadili msimamo wake ambao unaiweka nchi yake katika hatari ya kurejea katika machafuko.

REUTERS/Egyptian Presidency/Handout
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa kupigiwa kura kwa rasimu ya katiba unakuja wakati Wakristo na Waliberali wakilalamika kuwa baraza linaloratibu upatikanaji wa katiba linatawaliwa zaidi na waislamu ambao ni wanachama wa chama cha Muslim Brotherhood cha Rais Mohamed Mursi.

Mkuu wa baraza la katiba Hossam al Gherian alitoa wito kwa wakristo na Waliberali waliosusia majadiliano hayo kurejea katika mazungumzo ya leo alhamisi ili kukamilisha mapendekezo yatakayopelekwa kwa rais Mursi.

Watetezi wa haki za binadamu wamekosoa hatua ya kuharakishwa kwa upatikanaji wa katiba na wanaona hatua hiyo huenda ikasababisha kasoro nyingi katika katiba inayoandaliwa.

Juma lililopita rais Mursi alijiongezea madaraka uamuzi uliopingwa na idara ya mahakama, wanasiasa na wananchi wengine na kusababisha maandamano makubwa nchini humo na mwenyewe ameahidi kuachia madaraka hayo pindi katiba mpya itakapokamilika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.