Pata taarifa kuu
DRCongo

Serikali ya DRC yasema haikubaliani na ombi la waasai kutaka wapewe utawala wa Goma

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC imesema haiwezi ikakubaliana na ombi la Kundi la Waasi la M23 ambalo linataka kupewa Utawala wa Mji wa Goma na kusema wamedhibiti kila kitu katika eneo hilo hata kama waking'ang'ania kulishikilia. 

RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Habari na Mawasiliano ambaye pia ni Msemaji wa Serikali ya Kinshasa Lambert Mende Omulanga amesema Waasi wa M23 hawana uwezo wa kukabiliana na mikiki ambayo ipo katika Mji wa Goma.

Gilbert Kalinda ni Mbunge wa Kitaifa wa Kivu Kaskazini kwa upande wake amesema wao hawapendezwi na kile ambacho wanakishuhudia kikitendeka katika eneo la Mashariki mwa DRC.

Wananchi wa eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wameendelea kuishi kwa wasiwasi kutokana na kutokuwa na uhakika kama Kundi la Waasi la M23 halitarejea tena Goma.

Katika hatua nyingine kundi la Waasi la M23 limeanza kutupa lawama kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuwa inahusika na suala la uuzaji wa silaha kwa makundi ya Waasi huku wakisema wapo tayari kuondoka Goma.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.