Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na rais Zuma yatupiliwa mbali

Jaji mmoja nchini Afrika Kusini ametupilia mbali ombi la upande wa upinzani nchini humo la kutaka bunge lifanye kikao cha dharura cha kujadili kuhusu kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, ambapo chama tawala nchini humo ANC kinapinga pia hatua hiyo. 

orgellaonline.com
Matangazo ya kibiashara

Jaji huyo amesema sheria za bunge nchini humo haziko wazi kuhusu utatuzi wa mzozo wakati wabunge wa chama tawala wakiwa wengi kupinga ombi la upinzani, na sio jukumu la mahakama kuingilia kati.

Vyama vinane vya upinzani, vimelitaka bunge la Afrika Kisini kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais Jacob Zuma kwa tuhuma za kushindwa kutatua matatizo yanayo likumba taifa hilo, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira, rushwa, uingiliaji wa siasa katika masuala ya sheria pamoja na mdororo wa uchumi wa taifa hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.