Pata taarifa kuu
MALI

Kundi la Waasi la MUJAO lasherehekea ushindi dhidi ya waasi wa Tuareg,nchini Mali

Wapiganaji wa kundi la kiislamu la MUJAO kaskazini mwa Mali wamevurumisha risasi hewani ishara ya kufurahia ushindi dhidi ya wapiganaji wa Tuareg wa MNLA baada ya kushuhudiwa mapigano makali siku ya ijumaa iliyopita katika mji wa Gao unaokaliwa na wapiganaji hao tangu mwezi June baada ya kuwafukuza wapiganaji wa MNLA.

Kundi la waasi wa Tuareg linalodaiwa kushindwa katika mapambano dhidi yake na kundi la waasi wa kiislamu MUJAO
Kundi la waasi wa Tuareg linalodaiwa kushindwa katika mapambano dhidi yake na kundi la waasi wa kiislamu MUJAO AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashahidi wamesema makundi ya wapiganaji wa MUJAO wakiwa katika msafara wa magari sita ya kijeshi waliingia katika mji wa Gao huku wakirusha risasi hewani wakati wakitokea kwenye uwanja wa mapambano.

Kiongozi mmoja wa kundi la MUJAO Abou Dardar amethibitisha kuwa wamewashinda wapiganaji wa MNLA.

Duru za kiusalama nchini Mali na Burkinafaso zinaarifu kuwa naibu kiongozi wa jeshi la MNLA kanali Mechkanine amejeruhiwa katika mapigano hayo.

Hayo yanajiri wakati mawaziri wa ulinzi kutoka umoja wa ulaya wanataraji kukutana leo pamoja na katibu wa majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi NATO Anders Fogh Rasmussen kuzungumzia mzozo wa Mali na uwezekano wa kutuma kikosi cha kijeshi cha umoja wa ulaya kwa ajili mafunzo ya wanajeshi wa Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.