Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE

Sierra Leone yashuhudia uchaguzi kwa mara ya tatu tangu kumalizika kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe

Wapiga kura nchini Sierra Leone wanaingia katika zoezi la uchaguzi kwa mara ya tatu tangu kumalizika kwa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe na kushuhudia takribani vyama nane vya siasa vikisimamisha wagombea kuwania nafasi ya uraisi na kumi vikishiriki katika uchaguzi wa wabunge.

Mgombea wa uraisi nchini Sierra Leone kutoka chama cha upinzani Julius Maada Bio akiwa katika moja ya harakati za kampeni zake nchini Sierra Leone
Mgombea wa uraisi nchini Sierra Leone kutoka chama cha upinzani Julius Maada Bio akiwa katika moja ya harakati za kampeni zake nchini Sierra Leone Reuters/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la uchaguzi wa uraisi,wabunge na viongozi wa ngazi za chini linasimamiwa chini ya jumuiya ya kimataifa ambayo imelisaidia taifa hilo la Afrika magharibi kusimama upya baada ya takribani muongo mzima wa machafuko.

Wakati bado ni moja ya mataifa maskini zaidi duniani, Sierra Leone imejaliwa utajiri katika rasilimali za madini kama chuma ambapo inakadiriwa kuongeza pato la ndani la nchi hiyo kwa asilimia 21 kwa mujibu wa shirika la fedha duniani IMF.

Huu unakuwa uchaguzi wa kwanza kufanyika chini ya serikali ya siera leon na kuweka kumbukumbu ya uchaguzi wa kwanza wa uraisi,ubunge na viongozi wa ngazi za chini kufanyika pamoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.