Pata taarifa kuu
Somalia

Bunge la Somalia laidhinisha Baraza la Mawaziri baada ya kupendekezwa na Waziri mkuu

Bunge Jipya nchini Somalia limeliidhinisha Baraza Jipya la Mawaziri ambalo limependekezwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo tayari kuanza majukumu yao ya kuongoza serikali.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Wabunge mia mbili na kumi na tisa kati ya mia mbili ishirini na tano wamepiga kura ya ndiyo kuidhinisha Baraza Jipya la Mawaziri ambalo linaanza kazi ya kulijenga Taifa hilo lililopitia kwenye miongo miwili ya vita.

Spika wa Bunge Mohamed Osman Jawari ndiye ambaye ametangaza matokeo hayo ambayo yameidhinisha Baraza hilo la Mawaziri lenye Mawaziri kumi wakiwemo wanawake wawili kwa mara ya kwanza katika historia ya Somalia.

Mawaziri hao wawili wanawake ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Fowsiyo Yusuf Haji Adan ambaye atakuwa na jukumu la kuifanya nchi hiyo kuwa na mahusiano mema na mataifa mengine ya nje.

Wabunge wamepitisha Baraza hilo Jipya la Mawaziri lakini wamekiri mawaziri hao watakuwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha wanatimiza malengo ambayo wamejiwekea katika kuijenga nchi hiyo baada ya vita vya muda mrefu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.