Pata taarifa kuu
RWANDA-DRC-UN

Majeshi ya Rwanda na Congo DR yatunishiana misuli mpakani

Mpambano baina ya Kundi la Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na wenzao wa Rwanda yameripotiwa kuzuka katika eneo la mpaka wa nchi hizo mbili kitu ambacho kinaongeza hofu ya usalama baina ya nchi hizo mbili.

Msemaji wa jeshi la Rwanda, Joseph Nzabamwita amethibitisha kutokea kwa mapigano baina ya majeshi ya Rwanda dhidi ya Congo DR
Msemaji wa jeshi la Rwanda, Joseph Nzabamwita amethibitisha kutokea kwa mapigano baina ya majeshi ya Rwanda dhidi ya Congo DR rwandarwiza.unblog.fr
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi la Rwanda Joseph Nzabamwita amesema mapambano hayo yalizuka baada ya wanajeshi wao kuwaona wale wa DRC wakiwa wameingia katika mipaka yao kwa lengo la kufanya upelelezi ndipo mashambulizi yakatokea.

Serikali ya Kinshasa yenyewe imekanusha kuwepo kwa mapambano ya makundi ya jeshi na badala yake Msemaji wa Jeshi lake FARDC Kanali Olivier Hamuli amesema alikuwa ni mwanajeshi mmoja.

Mapambano hayo yalizuka jirani na mji wa Goma nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo katika jimbo la kivu kaskazini ambapo jeshi la serikali ya Congo DR limekuwa katika mapambano dhidi ya wapiganaji waasi wanaongozwa na kundi la M23.

Serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo pamoja na umoja wa mataifa wameituhumu Rwanda kwa kuunga mkono wapiganaji waasi madai ambayo serikali ya Kigali imeyapinga vikali.

Serikali ya Rwanda nayo imedai kuwa kinshasa imekuwa ikisaidia waasi wa FDLR kundi linaloundwa na wapiganaji wakihutu ambao walikuwa wanajeshi katika jeshi la Rwanda kabla kufukuzwa nchini humo baada ya mauaji ya halaiki mwaka 1994.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.