Pata taarifa kuu
NIGERIA

Jeshi nchini Nigeria lalaumiwa kwa kukiuka Haki za Binadamu kwenye kampeni yao dhidi ya Boko Haram

Jeshi la Polisi nchini Nigeria limeingia kwenye lawama ya kukiuka haki za binadamu kwenye kampeni yao ya kupambana na Kundi la Waislam wenye Msimamo Mkali la Boko Haram ripoti ya Shirika la Amnesty International inaeleza.

Wanajeshi wa Nigeria wakiwa kwenye eneo la Damaturu baada ya Kundi la Boko Haram kutekeleza shambulizi
Wanajeshi wa Nigeria wakiwa kwenye eneo la Damaturu baada ya Kundi la Boko Haram kutekeleza shambulizi Leadership Newspaper
Matangazo ya kibiashara

Amnesty International kwenye ripoti yake inaweka bayana makosa ambayo yanafanywa na Jeshi nchini Nigeria ikiwemo ni pamoja na kutekeleza mauaji, kutumia nguvu kubwa wakusambaratisha watu pamoja na kutesa raia.

Ripoti hiyo ya Shirika la Amnesty International licha ya kulituhumu Jeshi la Nigeria lakini imeelekeza lawama zake kwa Kundi la Boko Haram kutokana na kutekeleza mauaji ya kikatili ikiwa ni pamoja na kuchoma makanisa na shule.

Boko Haram kwenye ripoti hiyo linatuhumiwa pia kwa kufanya mashambulizi dhidi ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiwaandika vibaya kitu ambacho ni kinyume na haki za binadamu.

Amnesty International kwenye ripoti yake inaonesha Jeshi la Nigeria limekuwa likikiuka haki za binadamu kutokana na kukamata watu ambao si wanachama wa Kundi la Boko Haram na kuwatesa.

Jeshi nchini Nigeria kupitia Msemaji wake Kanali SK Usman limekanusha madao ambayo yameorodheshwa kwenye ripoti hiyo ya Amnesty International na kusema wanajeshi wao wamekuwa wakifuata weledi.

Kanali Usman amesema hakuna mwanajeshi wa nchi hiyo ambaye anapelekwa kwenye kampeni hiyo kwa lengo la kuua raia wasio na hatia kama ambavyo imekuwa ikielezwa kwenye ripoti hiyo.

Msemaji huyo wa Jeshi amesema kila ambacho kinafanyika kwenye kampeni ya kupambana na Kundi la Boko Haram kinajiegemeza katika kuhakikisha sheria hazivunjwi kwa namna yoyote ile.

Shirika la Amnesty International limetoa ushauri kwa serikali kuhakikisha linatoa ushahidi pindi linapolituhumu Kundi la Boko Haram kutekeleza shambulizi la aina yoyote kitu ambacho kitasaidia kuondolewa kwa malalamiko haya.

Kundi la Boko Haram tangu mwaka 2009 limekuwa likitekeleza mashambulizi dhidi ya serikali wakitaka kuwepo na matumizi ya sharia na kuachana na elimu ya magharibi wanayodai imejaa upotoshaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.