Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Jeshi la Polisi nchini Afrika Kusini latumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwasambaratisha wachimbaji wa Mgodi wa Anglo American Platinum

Jeshi la Polisi nchini Afrika Kusini limetumia mabomu ya machozi, risasi za mpira na magurunedi ya bandia kupambana na wafanyakazi wa Mgodi wa Anglo American Platinum waliofukuzwa kazi mapema mwezi uliopita.

Polisi nchini Afrika Kusini wakiwa wamejihami kwa silaha kukabiliana na wafanyakazi wa Mgodi wa Anglo American Platinum
Polisi nchini Afrika Kusini wakiwa wamejihami kwa silaha kukabiliana na wafanyakazi wa Mgodi wa Anglo American Platinum
Matangazo ya kibiashara

Mapambano hayo baina ya wafanyakazi wa Mgodi wa Anglo American Platinum na jeshi la Polisi yalitokea baada ya muda wa mwisho uliowekwa kwa wachimbaji hao kuondoka katika eneo la mgodi kumalizika nao wakakaidi amri hiyo.

Mgodi wa Anglo American Platinum ulifikia uamuzi wa kuwatimua kazi wafanyakazi wake 1200 mapema mwezi uliopita lakini wafanyakazi hao wamerejea tena na kudai kurejeshwa kazini.

Mapema kabla ya kuzuka mapambano baina ya Polisi na wafanyakazi hao asubuhi wafanyakazi zaidi ya elfu moja wa Mgodi wa Anglo American Platinum walifika eneo hilo na kuzuia njia huku wakichoma moto.

Msemaji wa Polisi nchini Afrika Kusini Dennis Adriao amethibitisha kutumika kwa mabomu ya machozi na risasi za mpira kwenye ghasia hizo na wakafanikiwa kuwatawanya zaidi ya wachimbaji 1000.

Adriao ameweka bayana walilazimika kutumia nguvu kubwa zaidi kutokana na wachimbaji hao kuzuia njia na kuchoma mota ambao ulianza kuwa kitisho kwa watu ambao walikuwa wanaelekea katika Mgodi wa Anglo American Platinum.

Wafanyakazi wa migodini nchini Afrika Kusini wamekuwa mstari wa mbele kuendesha migomo wakishinikiza kupatiwa nyongeza ya mshahara kitu ambacho kilionekana kukwamisha uzalishaji na hivyo wakatimuliwa kwenye Mgodi wa Anglo American Platinum.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.