Pata taarifa kuu
LIBYA

Waziri Mkuu wa Libya aachia ngazi aada ya uteuzi wa baraza mawaziri kukataliwa na Bunge

 Waziri mkuu wa Libya Mustafa Abu Shagur ameondolewa kwenye nafasi yake na bunge la congres la nchi hiyo baada ya baraza lake la mawaziri alilolitangaza kwa mara ya pili siku ya Jumapili kukataliwa na wabunge.  

Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Wabunge walikuwa wamempa waziri mkuu Shagur saa sabini na mbili awe amewasilisha serikali mpya baada ya ile ya awali pia kukataliwa na bunge hatua ambayo sasa imemlazimu kiongozi huyo kuachia nafasi yake.

Hasanaa Alamini ni mbunge wa kujitegemea kutoka Misrata na amesema kuwa hatua ya kuondolewa kwa Waziri mkuu Shagur haimanishi kuwa nchi hiyo itaingia kwenye machafuko.

Kufuatia hatua hiyo bunge linalazimika kuchagua waziri mkuu mpya ili kuchukua nafasi ya kiongozi huyo ndani ya kipindi cha wiki tatu mpaka nne kwa mujibu wa sheria.

Hatua ya kutimuliwa kibaruani kwa waziri mkuu huyo ilikubaliwa na kusainiwa na wabunge wapatao 126 kati ya 186 ya wabunge waliokuwa ndani ya bunge hilo ambalo lina jumla ya viti vya 200.

Moja ya mambo yaliyokuwa yakipingwa katika uteuzi wake wa baraza la mawaziri ni uteuzi wa kanali aliyeoongoza harakati za kumng'oa dikteta Muammar Gaddafi na kupewa nafasi ya waziri wa Ulinzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.