Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI

Ufaransa kuwasilisha maazimio mawili UN kuhusu amani nchini Mali

Serikali ya Ufaransa inatarajia kuwasilisha maazimio mawili mbele ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa UN Kuhusu suala la amani nchini Mali.

Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa mataifa Gerard Araud
Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa mataifa Gerard Araud RFI
Matangazo ya kibiashara

Moja ya maazimio,ni kuomba kuwepo majadiliano ya kisiasa baina ya serikali ya Bamako na Makundi ya wapiganaji waasi walioko kaskazini mwa nchi hiyo,huku azimio la pili likiwa kuruhusiwa kwa kikosi cha kimataifa cha wanajeshi wa kulinda amani.

Kwa upande wake balozi wa Ufaransa ndani ya Umoja wa Mataifa, Gerard Araud amesema kuwa huu ndio wakati ulio mwafaka kwa baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuchukua hatua kuhusu nchi hiyo ya Mali.

Hayo yanajiri wakati viongozi wa jumuia ya maendeleo ya kiuchumi kutoka nchi za Afrika magharibi Ecowas,wakiweko wawakilishi wa umoja wa afrika pamoja na Umoja wa Ulaya wakitazamiwa kukutana mjini Bamako nchini Mali,kujadili Mustakabali wa taifa hilo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.