Pata taarifa kuu
Sudan

Ban Ki Moon ataka uchunguzi wa kina kuhusu vifo vya wanajeshi wa UNAMID nchini Sudan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anataka uchunguzi wa kina kufanyika kuhusu mashambulizi dhidi ya wanajeshi wanne wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Matangazo ya kibiashara

Ban ameitaka serikali ya Khartoum kuhakikisha kuwa uchunguzi huo unafanyika kwa njia ya wazi ili wahusika kuchukuliwa hatua ya kisheria kwa kutekeleza mauaji hayo.

Wanajeshi hao wa UN waliouawa walikuwa raia kutoka Nigeria na walishambuliwa na watu wasiojulikana Kilomita mbili kutoka katika makao yao makuu katika mji wa Geneina.

Zaidi za wanajeshi elfu 16 kwa sasa wako katika jimbo la Darfur kuwalinda raia wa Sudan tangu mwaka 2007 na wanajeshi 78 wameuawa tangu kuanza kwa oparesheni hiyo.

Jimbo la Darfur kwa zaidi ya miaka 10 limekuwa likikabiliwa na ukosefu wa usalama kutoka kwa makundi ya waasi kupanga mashambulizi dhidi serikali ya Khartoum.

Ojwang Agina ni mchambuzi wa siasa za Sudan yeye ameiambia RFI Kiswahili kuwa mauaji hayo huenda yalipangwa na serikali ili kuonesha kuwa haiungi mkono wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa kuwa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.