Pata taarifa kuu
Nigeria

Wanafunzi zaidi ya 20 wauliwa kwa kupigwa risasi Nigeria

Kundi la watu lililokuwa limejihami kwa bastola nchini Nigeria limewaua zaidi ya wanafunzi 20 baada ya kuwapiga  risasi  katika Chuo kimoja cha mafunzo ya juu mjini Mubi katika jimbo la Adamawa. 

Matangazo ya kibiashara

Walioshuhudia mkasa huo wanasema wanafunzi hao walipigwa risasi wakiwa katika mabweni yao huku kiini cha shambulizi hilo kikiwa bado hakijafahamika wala kundi hilo kutambuliwa.

Mhadhiri mmoja katika chuo hicho ambaye hakutaka kutambuliwa amesema watu hao waliwaamuru wanafunzi hao kupiga foleni na kuwataka kutaja majina yao kabla ya kuanza kuwafwatulia risasi .

Akizungumza na idhaa ya BBC Hausa, Mhadhiri huyo alisema baadhi ya wanafunzi walidungwa visu kabla ya watu hao kutoroka.

Watu wanaoishi karibu na chuo hicho nao wanasema walisikia milipuko ya bastola usiku kucha na kuingiwa na hofu kuhusu kilichokuwa kinaendelea katika chuo huku wengi wakihofia maisha yao.

Mamlaka katika mji huo wa Mubi umetoa amri ya kutotoka nje kutokana na shambulizi hilo ambalo ni baya zaidi kuwahi kuwakumba wanafunzi nchini Nigeria.

Serikali nchini Nigeria imekuwa ikikabiliwa na hali ngumu ya kiusalma kutoka kundi la Boko Haram ambalo makao yao ni Kaskazini mwa taifa hilo kwa kusababisha vifo vya watu kwa kuwashambulia.

Shambuzli hili linakuja siku moja tu baada ya rais Goodluck Jonathan kuwaahidi raia wa nchi hiyo kuwa serikai yake inafanya kila kinachowezekana kuimarisha usalama nchini humo na kukabiliana na Boko Haram.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.