Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Wachimbaji wa madini wa mgodi wa Marikana nchini Afrika Kusini wamerejea kazini baada ya mgomo wa majuma sita

Maelfu ya wachimbaji wa madini kwenye mgodi wa Lonmin Marikana nchini Afrika Kusini wamerejea kazini hii leo baada ya mgomo wao wa majuma sita ambao umefanikisha kupata nyongeza ya mshahara kwa asilimia ishirini na mbili.

Wachimbaji wa madini katika mgodi wa Marikana nchini Afrika Kusini ambao wamerejea kazini hii leo
Wachimbaji wa madini katika mgodi wa Marikana nchini Afrika Kusini ambao wamerejea kazini hii leo REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Wachimbaji hao wa madini wamerejea kazini baada ya hiyo jana kuendelea kupambana na polisi ambao walikuwa wanawasambaratisha wasifanye maandamano baada ya suala la nyongeza ya mshahara kuafikiwa.

Wachimbaji hao wa mgodi wa Marikana ambao unatajwa kama kitovu cha mgomo na maandamano kwenye sekta ya madini uliosababisha hasara ya zaidi ya dola bilioni moja wamerejea na kuonekana wakiwa na furaha.

Baadhi ya wachimbaji hao wameonekana wakisema wazi wazi wataendelea kudai maslahi yao kila pale inayoonekana inafaa bila ya kutishwa na kitu chochote na wala nguvu ya jeshi la polisi.

Wachimbaji hao wameweka bayana kwa nyongeza hii ya malipo itawafanya waweze kujikimu kimaisha tofauti na hali ambayo ilikuwa hapo awali kwani walikuwa wanapata malipo madomo mno.

Wachimbaji wa madini nchini Afrika Kusini walijiapiza kutorejea kazini hadi wapate nyongezo kutokana na kuelewa na mzigo wa kuendesha familia zao kutokana na maisha kuwa ghali huku mshahara ukiwa mdogo.

Wachimbaji arobaini na sita wa mgodi wa Marikana walipoteza maisha kwenye vugvugu la kudai nyongeza ya mshahara na maboresho ya mazingira ya kazi kitu kilichoongeza hasira kwa wenzao kuendelea na mgomo.

Kampuni ya Anglo American Platinum imetoa tangazo la kutishia kuchukua hatua kwa wafanyakazi ambao watashindwa kurejea kazini hii leo wakisema ni wajibu kwa kila mfanyakazi kuendelea na kazi baada ya kupatikana kwa muafaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.