Pata taarifa kuu
Nigeria

Kundi la Boko Haram lakiri kuharibu Nguzo za Mawasiliano ya simu Kaskazini mwa Nigeria

Kundi la kiislam la Boko Haram limedai kuharibu nguzo za mawasiliano ya simu katika eneo la kaskazini mwa Nigeria, na kutishia waandishi wa Habari.

Wafuasi wa Kundi la Boko Haram la nchini Nigeria
Wafuasi wa Kundi la Boko Haram la nchini Nigeria AFP PHOTO / YOUTUBE
Matangazo ya kibiashara

Nguzo kadhaa za mitandao ya Simu zilichomwa moto, yakiwa ni mashambulio mapya kutekelezwa na Kundi hilo ambalo limekuwa likitekeleza Mashambulizi ya Risasi na Mabomu.
 

Kundi hilo limedai kufikia hatua hiyo kwa kile walichoeleza kuwa ni kutokana na mitandao hiyo kutoa msaada wa Taarifa juu ya Kundi la Boko Haram kwa Mawakala wa usalama Taarifa zinazopelekea kukamatwa kwa Wafuasi wa Kundi hilo.
 

Mkuu wa Jeshi la Polisi alitoa amri ya kufanyika uchunguzi wa Saa 24 kutokana na tukio hilo.
 

Kundi la Boko Haram linashutumiwa kusababisha vifo vya Watu zaidi ya 1,400 kaskazini na katikati mwa Nigeria tangu Mwaka 2010.
 

Boko Haram awali ilitishia Vyombo vya Habari vya Sauti ya Amerika, Idhaa ya Radio ya nchini Ufaransa iliyoko nchini Nigeria pia Gazeti Mashuhuri nchini humo, This Day.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.