Pata taarifa kuu
Afrika Kusini

Mahakama nchini Afrika kusini kuwaachia huru wafanyakazi 270 wa Mgodi wa Markana waliokuwa wakishikiliwa

Mahakama nchini Afrika Kusini inatarajiwa kuanza kuwaachia huru Wafanyakazi wa mgodini 270 waliokamatwa na Polisi baada ya Polisi kuwashambulia kwa risasi Wafanyakazi 34 hatua ambayo ilifikiwa baada ya waendesha mashtaka kuwaondolea mashtaka ya mauaji ya Wafanyakazi hao.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza na Wafanyakazi wa Mgodi wa Marikana
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza na Wafanyakazi wa Mgodi wa Marikana REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Waendesha mashataka walifikia hatua hiyo hapo jana kufuatia ghadhabu iliyooneshwa na Raia nchini humo dhidi ya Askari waliowafyatulia risasi wafanyakazi wa Mgodi wa Marikana, tukio linaloelezwa kuwa baya zaidi kutekelezwa na askari tangu kumalizika kwa ubaguzi wa Rangi.
 

Siku ya ijumaa juma lililopita Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini aliwataka waendesha mashtaka kueleza kwa nini waliwakamata wafanyakazi hao na kuwashtaki kuwaua wenzao ilhali ilifahamika wazi kuwa Polisi walitekeleza kitendo hicho.
 

Akizungumza jana Mkurugenzi wa mashtaka Nomgcobo Jiba amesema uamuzi wa Mwisho juu ya uwezekano wa kuwafungulia mashtaka utachukuliwa baada ya kufanyika uchunguzi wa kina juu ya mauaji hayo.
 

Uchunguzi huo unatarajiwa kufanywa na Tume ya uchunguzi iliyoteuliwa na Rais Jacob Zuma ambayo imepewa mpaka mwezi Januari kuwasilisha matokeo ya Uchunguzi wake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.