Pata taarifa kuu
Afrika Kusini

Rais Zuma atishia kuzinyang'anya leseni kampuni zinazochimba madini Afrika Kusini

Rais wa afrika Kusini Jacob Zuma amewaonya wamiliki wa kampuni za kuchimba madini nchini humo kuwa huenda wakanyang'anywa leseni zao ikiwa hawataweka makazi mazuri kwa wafanyikazi wao.

REUTERS/Kopano Tlape/Government
Matangazo ya kibiashara

Aidha Zuma amezitaka kampuni hizo kusikiliza kilio cha wafanyikazi wao na kuwaongezea msharara kutokana na kupanda kwa gharama za maisha nchini humo .

Rais Zuma ameyasema haya wiki moja baaafay ya polisi kuwapiga risasi na kuwauwa wafanyiakzi 34 a mgodi waliokuwa wanakabaliana na polisi kuonyesha gadhabu zao za kutaka kuongezewa mishahara.

Wakati huohuo maelfu ya wananchi wa mji wa Marikana ulipo mgodi wa Platinum unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin wanafanya sherehe maalumu jirani na uwanja ulipo mgodi huo kwa ajili ya mazishi ya wenzao 34 waliouawa na polisi juma lililopita.

Sherehe za kimila zimeanza leo asubuhi kwa viongozi wa kijadi kuzungumza na familia za wachimba madini waliopteza ndugu zao wakati wa vurugu za wafanyakazi wa mgodi huo kudai nyongeza ya mishahara.

Baadae viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali watajumuika kwenye sherehe hizo kwa mazishi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.