Pata taarifa kuu
Ethiopia

Mwili wa Zenawi wawasili Ethiopia, viongozi duniani wamlilia

Mwili wa Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi umewasili nchini humo na kupokelewa na maelfu ya wananchi wa Ethiopia mjini Addis Ababa. Baada ya kuwasili mwili wake ulipelekwa katika makaazi yake ya kitaifa ambao umehifagdili wakati mipango ya mazishi ikiendelea.

REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Zenawi mwenye umri wa miaka 57 alifariki dunia mjini Brussles nchini ublegiji akipokea matibabu na kifo chake kinanednelea kuoombolezwa duniani.

Jeneza lilokua limebeba mwili wa marehemu Zenawi lilipelekwa makao rasmi ya waziri mkuu ndani ya ikulu ya Ethiopia na mwili utaendelea kuwa huko mpaka siku ya mazishi.

Televisheni ya Taifa hilo ilionyesha tukio hilo moja kwa moja huku maelfu ya waombolezaji wakishuhudia jeneza la kiongozi huyo likipita katika mitaa mbalimbali katika mji wa Addis Ababa.

Seriakli ya Ethiopia imetangaza maombolezo ya kitaifa lakini bado haijatangaza siku ya mazishi ya marehemu Zenawi huku ikieleza kuwa hali ya mambo ni shwari.

Viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wametuma salamu za rambirambi huku Rais wa Marekani Barack Obama akimwelezea Zenawi kama kiongozi anayestahili kutambuliwa kwa mchango wake wa muda mrefu wa kuleta maendeleo nchini Ethiopia na kupambana na umasikini.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton ameelezea kusikitishwa kwake na kifo cha Zenawi na kwamba anaamini kuwa Ethiopia itapita katika kipindi cha mpito cha uongozi kwa amani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa Zenawi alikuwa kiongozi wa kipekee barani Afrika wakati Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema Zenawi alipendwa sana nchini mwake na alikuwa rafiki wa karibu wa Israeli.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.