Pata taarifa kuu
Sudan Kusini-Ethiopia

Waasi wa Sudan Kusini wauawa Ethiopia, bomu lalipuka Ubalozi wa Misri nchini Libya

Mamlaka nchini Ethiopia zimesema kuwa zimewaua wapiganaji 16 toka kundi la waasi wa Sudan Kusini waliokuwa wamezuia njia kwenye mji wa Gambella kuelekea Sudan Kusini.

RFI
Matangazo ya kibiashara

 

Msemaji wa Serikali kwenye mji huo Omot Odeng Olol amesema kuwa wapiganaji hao mara baada ya kutakiwa kusalimisha silaha zao walikataa kutii amri ya polisi na badala yake walianza kuwashambulia na kusababisha vifo vya watu 16.

Mji huo umeshuhudia mapigano ya mara kwa mara ingawa tukio la juma lililopita halikuhusishwa na machafuko ambayo yameshuhudiwa kwa miezi kadhaa kwenye mji wa Gambella.

Ikiwa ni siku mbili zimepita toka kutokea kwa mlipuko wa bomu kwenye mji wa Tripoli nchini Libya, siku ya jumatatu kumeripotiwa mlipuko mwingine kwenye mji wa Benghazi aambapo hakuna watu waliojeruhiwa wala kupoteza maisha.

Polisi kwenye mji wa Benghazi wamethibitisha kutokea kwa mlipuko huo nje ya ofisi za ubalozi wa Misri, ambapo gari moja lililokuwa limeegeshwa nje ya ofisi hizo lililipuka lakini hakukuwa na mtu wakati huo.

Tayari polisi mjini tripoli imetangaza kuwashikilia watu 42 wanaotuhumiwa kuwa ni wafuasi wa marehemu kanali Muamar gaddafi amabo wamekuwa wakiendesha mashambulizi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.