Pata taarifa kuu
MALI

ECOWAS yajadili kupeleka wanajeshi Kaskazini mwa Mali

Viongozi wa majeshi kutoka muungano wa mataifa ya Afrika Magharibi, wanakutana mjini Bamako Mali kujadili uwekezano wa kutuma vikosi vya kijeshi Kaskazini mwa nchi hiyo kukabiliana na makundi ya kiislamu ambayo yamejitangazia uhuru wa eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo pia unawashirikisha maafisa  kutoka Umoja wa Mataifa na unamalizika siku ya Jumatatu baada ya kufanyika kwa siku nne, kumalizia mkakata wa kutuma majeshi ya ECOWAS Kaskazini mwa Mali.

Awali, ECOWAS ilitangaza kuwa ilikuwa imeandaa vikosi vya majeshi elfu tatu kwenda Kaskazini mwa nchi hiyo lakini ilikuwa inasubiri idhini kutoka kwa Umoja wa Mataifa.

Mazungumzo kati ya waasi hao wa kiislamu na rais wa Burkinafaso Blaise Compaore hayakuzaa matunda huku makundi hayo yakianza kutumia mfumo wa kiislamu wa sharia.

Katika hatua nyingine, rais wa mpito wa Mali Dioncounda Traore amesema ana matumaini makubwa na Waziri  Mkuu wake Cheick Modibo Diarra na anaamini utendajikazi wake.

Traore amesema yeye pamoja na Waziri Mkuu wake wako katika mchakato wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kutokana na mpasuko wa uongozi unaoshuhudiwa katika taifa lao.

Rais na Waziri Mkuu nchini Mali wamekuwa wakinukuliwa wakitofautiana kuhusu  mfumo wa serikali ya Umoja wa kitaifa ambayo inastahili kuundwa kufikia mwisho wa wiki hii.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.