Pata taarifa kuu
Mali

Viongozi wa baraza la kiislam nchini Mali waelekea kaskazini kukutana na viongozi wa kundi la kiislam linalo kalia eneo hilo.

Ujumbe wa baraza la kiislam nchini Mali ukiongozwa na kiongozi wake Mahmoud Diko umeondoka jijini Bamako kuelekea kaskazini mwa Mali kukutana na waasi wa kundi la Ansar Dine kujaribu kuanzisha mazungumzo na kundi hilo la kijeshi linalo shikilia eneo la kaskazini mwa nchi hiyo tangu miezi minne sasa. Juhudi hizo zinajiri wakati siku ya Jumapili iliopita waasi hao wa kundi la kiislam wametekeleza amri ya kiislam ya kuwapiga mawe hadi kufa familia moja ilieshi bila ndoa.

Wapiganaji wa kundi la Ansar Dine kaskazini mwa Mali
Wapiganaji wa kundi la Ansar Dine kaskazini mwa Mali REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Alipowasili jijini Gao, Mahmoud Diko, Kiongozi wa baraza la Kiislam amekutana na wakuu wa vijiji na wakuu wa madini ambao wamepongeza juhudi za baraza la kiislam nchini humo kujaribu kuutanzua mzozo uliopo hasa kuhakikisha suluhu ya mzozo huo inapatikana kupitia mazungumzo badala ya mbinu za kijeshi.

Kiongozi wa kundi la kiislam la Ansar Dine Iyad Ag Ghali, amesema hajapokea taarifa kuhusu ujumbe huo, lakini amekiri kuwa tangu miezi kadhaa wamekuwa katika mawasiliano na viongozi wa baraza la Kiislam. Mwezi Mei iliopita kundi hilo la Ansar Dine linaloongozwa na Iyad Ag Ghali aliwaacha huru wanajeshi 160 wa jeshi la Mali bila kuomba fidia na wanajeshi hao wakakabidhiwa kwa wajumbe wa baraza la kiislam.

Kiongozi wa Ansar Dine amekuwa akithibitisha kuwa kundi lao halina mtazamo wa kutaka mjitengo wa kaskazini, kama ilivyo kwa wenzano wa Touareg, wao wanachokitaka ni matumizi ya mfumo wa sharia na uundwaji wa la kiislam nchini Mali.

wakati hayo yakiarifiwa, Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International wanajeshi walilokuwa wanaumuunga mkono rais wa zamani Amadou Toumani Toure aliyepionduliwa uongozini mapema mwaka huu wameendelea kuteswa nahaki zao kukiukwa.

Shirika hilo linaongeza kuwa baadhi ya wanajeshi hao pia hawajulikani walipo na wanashtumu wanajeshi waliotekeleza mapinduzi hayo kutekeleza mateso hayo.

Katika hatua nyingine msemaji wa serikali ya mpito nchini humo Hamdoun Toure amekanusha kuwa waziir Mkuu Cheik Mudibo Diarra anabaguliwa na rais Diancounda Traore katika mpango wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kabla ya tarehe 4 mwezi ujao kwa mujibu wamakubalinao waliyoafikiana na umoja wa matiafa ya Afrika Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.