Pata taarifa kuu
Mali

Mali kupeleka Malalamiko ya Uharibifu wa Kaskazini mwa Mali mbele ya Mahakama ya ICC

Mali inampango wa kupeleka ombi kwa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita,ICC kufanyia uchunguzi Mauaji yaliyotekelezwa na Makundi ya Watu wenye Silaha wanaodhibiti eneo la Kaskazini mwa Mali ambao wamekuwa wakishutumiwa kukiuka haki za Binaadam kwa kutekeleza vitendo vya ubakaji na kuwatumia watoto katika Jeshi.

Waasi wa Tuareg walio Kaskazini mwa Mali
Waasi wa Tuareg walio Kaskazini mwa Mali
Matangazo ya kibiashara

Jumuia ya Kimataifa imekuwa ikisikitishwa na kuongezeka kwa kasi kwa Machafuko wakati ambapo Makundi ya kiislam ikiendelea kudhibiti eneo kubwa la kaskazini huku Raia wakiathiriwa kutokana na hali hiyo.
 

Ikulu ya Marekani imeelezwa kusikitishwa kwake na hali inayoendelea huko Mali na Rais wa nchi hiyo Barrack Obama ameidhinisha kiasi cha dola za kimarekani Milioni 10 kama fedha za dharura kwa ajili ya kuwasaidia Raia walioathiriwa na Machafuko.
 

Juma lijalo Mali itashtaki rasmi juu ya Mauaji katika Eneo la Kaskazini mbele ya Mahakama ya ICC, huku mashirika ya kimataifa yamethibitisha Mauaji hayo,chanzo cha Habari kutoka Wizara ya Sheria kimethibitisha.
 

Mwendesha Mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa kuwa uharibifu unaoendelea katika Maeneo ya kihistoria ya Kaskazini mwa Mali ni uhalifu wa kivita na kuwa Mahakama inakusanya Taarifa juu ya swala hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.