Pata taarifa kuu
Sudan Kusini

Maelfu ya Raia wa Sudani kusini walio Sudan washerekea Uhuru huku wakiwa hawana uhakika lini watarejea nyumbani

Maelfu ya Raia wa Sudan Kusini wanaoishi Sudan wameadhimisha mwaka mmoja tangu nchi yao ilipojitenga na Sudan wakiwa na mashaka bila ya kufahamu ni lini watarudi nyumbani.

Rais wa Sudani kusini Salva Kiir
Rais wa Sudani kusini Salva Kiir REUTERS/China Daily
Matangazo ya kibiashara

Wengi wa raia hao wanasema wameshindwa kurudi nyumbani kwa kukosa pesa hata baada ya muda wa mwisho wa kuishi Sudan kukamilika tarehe 8 mwezi Aprili.
 

Nyumbani jijini Juba,Rais Salva Kiir aliwataka wananchi wake kushirikiana pamoja ili kujenga uchumi wao kwa pamoja huku akitangaza kuzindua mitambo miwli ya kuzalisha mafuta katika majimbo ya Upper Nile na Unity.
 

Kiir ameapa kupambana na Rushwa na kuondoka katika Mfumo wa kutegemea sana Msaada kutoka Mataifa ya nje na kujitegemea kiuchumi.
 

Nayo Serikali ya Marekani imetoa wito kwa Sudani kusini kufikia makubaliano na Sudan katika suala la Usafirishaji wa Mafuta ambayo Mapato yake ni muhimu sana kwa Taifa hilo changa.
 

Wakati taifa hilo likisherekea Mwaka Mmoja tangu kupata Uhuru, linakabiliwa na Changamoto kubwa ikiwemo swala la Miundombinu kama vile Barabara na kukosa Mfumo mzuri wa usambazaji Maji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.