Pata taarifa kuu
MALI-BURKINA FASO

Bunge nchini Mali limeridhia uvamizi wa kijeshi Kaskazini mwa nchi hiyo kuwakabili Wapiganaji wa Kiislam

Bunge nchini Mali limeridhia kufanyika kwa uvamizi wa kijeshi katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo lililochini ya umiliki wa Makundi ya Wapiganaji wa Kiislam na kutangaza matumizi ya sharia za kiislam, kufanya uharibifu wa urithi wa vitu za kitamaduni na kuwaondoa wananchi kwenye maeneo yenye utajiri wa madini.

Wapiganaji wa Kundi la Waislam wa MNLA ambao wamekuwa mstari wa mbele kushinikiza kujitenga kwa eneo la Kaskazini mwa Mali
Wapiganaji wa Kundi la Waislam wa MNLA ambao wamekuwa mstari wa mbele kushinikiza kujitenga kwa eneo la Kaskazini mwa Mali AFP PHOTO / MNLA
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ambayo imetolewa na Bunge nchini Mali imeeleza kuwa watawaomba wananchi waendelee kushikama na serikali ya mpito na kupinga hatua ya Makundi ya Kiislam yanayotaka kujitangazia uhuru wa eneo la Kaskazini.

Bunge limesema kama kutakuwa na mshikamano wa dhati basi ni wazi watafanikiwa kwenye mpango huo wa kuyasambaratisha Makundi ya Kiislam ambayo yameendelea kuwa kitisho kwa usalama wa eneo la Kaskazini kwa sasa.

Msimamo wa Bunge nchini Mali wa kutaka nguvu za kijeshi zitumike Kaskazini mwa nchi hiyo unakuja siku moja baada ya waandamanaji kujitokeza kwenye mitaa ya Jiji la Bamako na kutaka serikali ichukue hatua kuwadhibiti wapiganaji wa Kiislam.

Kwenye maandamano hayo Kiongozi wa Wananchi wa Kaskazini ambao wanaishi Bamako Oumar Maiga amesema iwapo jeshi kama halitaki kuingia vitani basi ni bora serikali ikawapa wao zana ili waweze kukomboa mipaka yao.

Mmoja wa Wabunge kutoka Upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo Nock Ag Attia amesema makabila yaliyopo huko ambayo ni Tuareg, Fulani na Songhai hawaungi mkono kwa namna yoyote kile kinachofanywa na Waasi wa Tuareg na makundi mengine ya Kiislam.

Katika hatua nyingine Rais wa Serikali ya Mpito Dioncounda Traore ambaye tangu ameshambuliwa Ikulu anaendelea kupatiwa matibabu nchini Ufaransa atahudhuria Mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS huko Burkina Faso.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso Djibrill Bassole amethibitisha Rais Traore kuhudhuria mkutano huo akitokea nchini Ufaransa lakini hajaweka wazi iwapo atarejea nchini mali au atarudi Paris kuendelea na matibabu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.