Pata taarifa kuu
SUDAN-SUDAN KUSINI

Mazungumzo ya amani Sudan na Sudan Kusini yamalizika bila suluhu

Mazungumzo yaliyodumu kwa juma moja baina ya wajumbe wa Sudan na jirani zao wa Sudan Kusini yamemalizika nchini Ethiopia bila ya kupatikana kwa suluhu juu ya suala ma mgogoro wa mipaka baina ya pande hizo mbili na suala la usalama.

REUTERS/China Daily
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayao yamesehindwa kupata suluhu na hivyo wajumbe kutoka pande zote wanarejea makwao kabla ya kurudi tena Addis Ababa baada ya juma moja kuendelea na juhudi za kuhakikisha mgogoro wa mipaka unamalizwa.

Mazungumzo haya yalirejea chini ya shinikizo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa waliotishia kuziweka vikwazo nchi hizo kama zisingerudi kwenye meza ya mazungumzo.

Wakati huohuo inatarifiwa maelfu ya wananchi wa Sudan wanadaiwa kunaswa kwenye majimbo yenye mapambano kati ya waasi wa nchi hiyo wanaopigana na vikosi vya serikali na kwamba wanahitaji haraka msaada wa kibinadamu na hii ni kwamujibu wa Umoja wa Mataifa.

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa UN imetoa ripoti kuelezea matatizo ambayo wananchi wa majimbo ya kusini mwa Darfur na Kordofan wanakabiliwa nayo na kwamba wasipopatiwa msaada wa haraka wa chakula au kuhamishwa wengi watapoteza maisha.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya wananchi hao na kutoa wito kwa serikali na waasi wa SPLM-N wanaopigana na serikali kumaliza tofauti zao ili kuruhusu wananchi walionaswa kupatiwa msaada.

Nchi ya Ethiopia inawahifadhi zaidi ya wakimbizi laki mbili wanaotokea nchini Sudan wakikimbia vita.

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.