Pata taarifa kuu
DRC

Umoja wa Mataifa kuchapisha ripoti ya tuhuma za Rwanda kusaidia waasi wa M23

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limekubaliana kuichapisha ripoti kuhusu mgogoro unaoendelea mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC dhidi ya majeshi ya Serikali na waasi wa M23.  

REUTERS/Philippe Wojazer (
Matangazo ya kibiashara

 

Ripoti hiyo ambayo itachapishwa huenda ikasaidia kuondoa utata wa tuhuma za Rwanda kuhusika kuwasaidia waasi hao wanaopambana na majeshi ya serikali.
Ndani ya ripoti inadaiwa kuna ushahidi wa kuonyesha nafasi ya Rwanda kuwasaidia waasi wa M23 tuhuma ambazo zimekuwa zikikanushwa vikali na serikali ya Paul Kagame.

Mapambano kati ya majeshi ya serikali ya Rais Joseph Kabila na M23 yamekuwa kitisho cha usalama wa raia na mali zao na maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao.

Serikali ya Kabila imeapa kupambana na kundi la M23 lenye wapiganaji wengi waliosai kutoka katika jeshi la serikali na kujiunga katika kundi hilo linaloongozwa na Bosco Ntaganda anayesakwa kwa udi na uvumba na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.