Pata taarifa kuu
Rwanda-DRCongo

Serikali ya DRCongo yaendelea na uchunguzi kuhusu Rwanda kufadhili uasi mashariki mwa nchi hiyo

Serikali ya Rwanda yaendelea kukana kuhusika kwake katika vurugu zinazoendelea mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo katika Mkoa wa kivu ya kaskazini ambako jeshi la Congo linapambana na waasi wa kundi la M23 linalo muunga mkono jenerali muasi Jean Bosco Ntaganda anaesakwa na mahakama ya uhalifu wa kivita ICC, katika mpaka baina ya nchi hizo mbili.

Jenerali muasi nchini DRCongo Jean Bosco Ntaganda
Jenerali muasi nchini DRCongo Jean Bosco Ntaganda
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Congo upande wake imeendelea kutowa ushahidi kuhusu ufadhili wa Rwanda kwa waasi hao wa kundi la M23 wanaomuunga mkono jenerali muasi Jean Bosco Ntaganda kwa kuthibitisha kuwa Mei 27 mwaka huu jenerali huyo muasi alikuwa nchini Rwanda katika kambi ya kijeshi ya Kinigi mpakani nwa nchi hizo mbili ambapo inaaminik akuwa alikuwa pamoja na jenerali mwingine wa Rwanda Alex Kagame afisaa nambari tatu wa uongozi wa majeshi ya Rwanda.

Waasi wa Rwanda waliotoroka kundi la M23 walipitia katika kambi hiyo kabla ya kusafirishwa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya mapambano. Serikali ya Congo imesema wapiganaji hao walitumia majengo ya idara ya utalii na nbunga za wanyama mali ya Rwanda ilio mpakani na DRCongo.

Tume ya mseto ilioundwa kuchunguza madai ya Congo, inayo jumuisha wajumbe wa Rwanda na Congo. Serikali ya Rwanda ilikataa kuwaruhusu wajumbe wa tume hiyo kuingia katika maeneo yanayo tajwa kuwa eneo la mafunzo kwa wapiganaji hao kabla ya kujiunga na kundi la M23.

Msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende amesema kwamba ilikuwa muhimu kutekeleza uchunguzi huo, badala ya kuendesha uchunguzi huo katika vikao ma ofisini, kuna majumba yaliotajwa ambayo ilikuwa inastahili wataalamu kutoka pande hizo mbili kwenda kuchunguza na baadae kutubitishia aidha kukanusha, amesema hayo msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.