Pata taarifa kuu
Kinsasha

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lasema limewaua waasi 200

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linasema limewauawa wanajeshi zaidi ya 200 walioasi katika jeshi la serikali mwezi Aprili mwaka huu, na kuanza kupigana na majeshi ya serikali Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ambayo imetolewa na jeshi jijini Kinsasha pia inaeleza kuwa wanajeshi 40 wa kundi la FARDC wameualiwa katika makabiliano hayo.

Waasi hao walioauwa ni wanajeshi wa zamani wa serikali wenye asili ya Kitutsi waliojiunga na jeshi la serikali mwezi Machi mwaka 2009 baada ya kuafikiana na serikali, ili kudumisha usalama Mashariki mwa nchi hiyo lakini wamejiondoa katika jeshi hilo kwa madai kuwa wanabaguliwa na serikali.

Mkuu wa majeshi Didier Etumba, ambaye ametoa takwimu hizo amesema kuwa waasi wengine 250 na 93 na wanajeshi wa serikali wamejeruhiwa katika mapambano hayo.

Aidha, Kinsasha inasema waasi 374 wamejisalimisha na kuerejea katika jeshi la serikali wakiwemo 25 wenye uraia wa Rwanda.

Nalo kundi la M 23 linalopambana na majeshi wa serikali linasema kuwa wanajeshi kadhaa wa serikali wamejiunga nao tangu mwezi Aprili.

Serikali jijini Kinsasha inasema wanajeshi hao wa zamani wanaongozwa na Bosco Ntaganda, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi la CNDP anayetafutwa na Mahakama ya Kimatifa ya ICC kwa tuhma za mauji na kusajili watoto katika jeshi lake.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linashtumu Rwanda kuwafadhili wapiganaji wa M 23 tuhma ambazo serikali jijini Kigali imepinga.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.