Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-SUDAN

Juba yaishutumu Khartoum kwa kukiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa

Wakati nchi ya Sudan Kusini ikitangaza kuondoa vikosi vyake kwenye mpaka wake na nchi ya Sudan, waziri wa habari nchini humo Benjamin Barnaba ameishutumu serikali ya Khartoum kwa kuendelea kushambulia baadhi ya maeneo yake. 

Wanajeshi wa Serikali ya Sudan wakishangilia mjini Bentiu
Wanajeshi wa Serikali ya Sudan wakishangilia mjini Bentiu REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo amesema kuwa nchi hiyo kuendelea kushambulia maeneo yake ni kwenda kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN lilitaka kusitishwa kwa mapigano kati ya nchi hizo mbili.

Kauli ya waziri wa habari wa Juba imejibiwa vikali na Serikali ya Khartoum ambayo imedai kuwa ina haki ya kujibu mashambulizi ya aina yoyote ambayo yanafanywa dhidi yake akidai kuwa kama kuna mashambulizi basi wanajeshi wa Juba watakuwa wameingia kwenye mpaka wa nchi yake.

Waziri Benjamin amesema kuwa mashambulizi mapya ya Sudan yametekelezwa siku ya jumanne na Jumatano kwenye miji ya Upper Nile na mashariki mwa mji wa Bahr al-Ghazal ambako watu kadhaa wameripotiwa kuuawa.

Umoja wa mataifa umetishia kuziwekea vikwazo nchi hizo mbili endapo zitaendelea kupigana kwenye mpaka wa nchi hizo ambapo umesema kuwa ili kupata suluhu ni lazima vikosi vyote viondolewe kwenye mipaka na mazungumza kuanza upya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.