Pata taarifa kuu
MISRI

Utawala wa Kijeshi Nchini Misri waeleza utayari wa kuondoka madarakani baada ya Uchaguzi wa Rais sambamba na kulaani vifo vilivyotokea

Utawala wa Kijeshi Nchini Misri umeahidi kuhakikisha Uchaguzi wa Rais nchini humo unafanyika kwa uhuru na haki na kisha watakabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia ambayo itachaguliwa baada ya kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika tarehe 24 May.

Meja Jenerali Mohammed Al Assar akitangaza utayari wa Utawala wa Kijeshi kuondoka madarakani baada ya Uchaguzi wa Rais 24 May
Meja Jenerali Mohammed Al Assar akitangaza utayari wa Utawala wa Kijeshi kuondoka madarakani baada ya Uchaguzi wa Rais 24 May
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa Kijeshi kupitia Meja Jenerali Mohammed Al Assar umelazimika kutoa hakikisho hilo sambamba na kulaani mashambulizi na vifo vilivyowakuta waandamanaji waliokuwa wameweka kambi nje ya Wizara ya Ulinzi wakitaka uwepo wa kikomo cha Utawala wa Kijeshi.

Meja Jenerali Al Assar amewaambia wanahabari kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha kwa asilimia mia moja uchaguzi wa rais nchini humo unaendeshea kwa misingi ya uwazi na ukweli huku wakikanusha tetesi ya uwepo wa wagombea waliowapandikiza.

Utawala wa Kijeshi umeweka bayana kupata barua kutoka Tume Huru ya Uchaguzi ambayo imeomba Wizara ya Mambo ya Nje kuwaalika Waangalizi wa Kimataifa 45 ili waende kushuhudia namna ambavyo zoezi hilo litafanyika.

Licha ya kuomba Waangalizi hao 45 lakini Tume ya Uchaguzi pia imetaka Wizara ya Mambo ya Nje kuomba wajumbe kutoka nchi nyingine pamoja na kuruhusu Mashirika matatu ya kigeni kushuhudia uchaguzi huo.

Jeshi pia limethibitisha watu 20 kupoteza maisha na wengine 160 wamejeruhiwa kwenye mapambano yaliyozuka baina ya waandamanaji hao wanaoshinikiza kikomo cha Utawala wa Kijeshi na hivyo kukabiliana na watu wenye silaha kabla wanajeshi hawajaingilia kati.

Utawala wa kijeshi chini ya Field Marshal Mohammed Hussein Tantawi umelazimika kutoa hakikisho jingine kwa wananchi kwa kuwaeleza wapo tayari kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia ambayo itachanguliwa baada ya uchaguzi wa tarehe 24 May.

Tangazo hilo linabatilisha kauli yake ya awali ambayo iliweka bayana lengo lake ni kuacia madaraka kwa serikali ya kiraia mnamo mwezi Juni lakini kutokana na kuongezeka kwa shinikizo wamebadili uamuzi.

Wagombea wanne wa nafasi ya urais nchini Misri wamelazimika kusitisha kampeni zao kutoa nafasi ya maombolezo baada ya kutokea kwa vifo hivyo vilivyongeza wasiwasi juu ya hali ya usalama.

Wagombea ambao wametangaza kusitisha kampeni zao ni pamoja na Abdel Moneim Abul Fotouh, Khaled Ali, Hamdeen Sabbahi na Amr Mussa ambao wamesema wameguswa na hivyo ambavyo vimetokea.

Mashambulizi haya yamekuja na kuchangia vifo na majeruhi huku Utawala wa Kijeshi ukiendelea kukutana na ukosoaji mkubwa kwani wananchi wanadai umeshindwa kuongoza nchi hiyo katika misngi sahihi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.