Pata taarifa kuu
SUDAN-SUDAN KUSINI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN lazitaka Sudan na jirani zao Sudan Kusini kusitisha mapigano yanayoendelea

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN limetaka mapigano baina ya Sudan na Sudan Kusini yasitishwe mara moja ili kutoa nafasi ya mazungumzo baina ya pande hizo mbili zinazohasimiana na kupigania mipaka ya maeneo yenye utajiri mkubwa wa mafuta katika eneo hilo.

Wanajeshi wa Sudan wakiwa kwenye doria katika eneo la mpaka na nchi ya Sudan Kusini
Wanajeshi wa Sudan wakiwa kwenye doria katika eneo la mpaka na nchi ya Sudan Kusini 照片来源:大赦国际网站
Matangazo ya kibiashara

Agizo la Baraza la Usalama ambalo limeidhinishwa na wanachama kumi na tano wa kudumu ambazo wameendelea kuhimiza kusitishwa kwa mapigano ambayo yanashuhudiwa kugombea eneo la Heglig ambalo Sudan na wenzao Sudan Kusini kila moja kwa upande wake inadai ni eneo lao.

Serikali ya Juba imeendelea kuishutumu Khartoum kutokana na kuendelea kufanya mashambulizi katika eneo la Bentiu licha ya uwepo wa miito mingi ya kimataifa kushinikiza ndege za Sudan kuacha kuendelea na operesheni yake ya kijeshi.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na mwenzake wa Sudan Omar Hassan Al Bashir wameendelea kutuhumiana kila mmoja na kila upande ukisema nchi nyingine ina lengo la kuazisha vita.

Msemaji wa Jeshi la Sudan Sawarmi Khaled Saad amekanusha madai ya Sudan Kusini ya kwamba majeshi ya Khartoum yamefanya mashambulizi matatu kwenye eneo la Heglig na kusema hizo ni shutuma zisizo na msingi.

Serikali ya Juba yenyewe imeendelea kusema haitoondoa vikosi vyake katika eneo la Heglig licha ya shinikizo la Kimataifa kuanza kutolewa kwa nchi hiyo kuhakikisha inaondoa majeshi yake katika eneo hilo.

Juba imesema iwapo mashambulizi ya Khartoum yataachwa yaendelea wao watapeleka vikosi vyao hadi eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei kulinda mipaka yake ambayo kwa sasa ipo hatarini.

Hofu ya kuibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya Sudan na Sudan Kusini imeongezeka kitu ambacho kimechangia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kushinikiza hali hiyo isitoshwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.