Pata taarifa kuu
Sudan-Sudani kusini

Ban Ki Moon ataka utulivu wakati mkutano wa nchi hizo mbili ukivunjika

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ametaka kuwepo kwa utulivu baada ya Mkutano uliokuwa ukitarajiwa kufanyika mwezi ujao kati ya Marais wa Sudan na Sudani kusini kuahirishwa kufuatia mapigano katika mpaka wa Nchi hizo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Habari wa Sudan Abdullahi Ali Massar amesema Serikali imesitisha safari ya Omar Al Bashir ya mjini Juba baada ya Jeshi la Sudani kusini kushambulia eneo tajiri la mafuta la Heglig.

Msemaji wa Ban Ki Moon, Martin Nesirky amezitaka Sudani na Sudani kusini kumaliza mapigano na kutii makubaliano yaliyotiwa saini juu ya usalama wa mipaka ya nchi hizo.

Mazungumzo yaliyokuwa yakitarajiwa kufanyika kati ya Bashir na Salva Kiir ni juu ya kuondokana na tofauti walizokuwa nazo zilizosukuma kuingia katika vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.