Pata taarifa kuu
Cairo

Maelfu ya waombolezaji wahudhuria ibada ya Askofu Mkuu wa kanisa la Coptic nchini Misri Shenuda wa III

Maelfu ya waombolezaji wamehudhuria ibada ya wafu ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Coptic nchini Misri Shenuda wa III,aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Matangazo ya kibiashara

Ibada ya kiongozi huyo aliyefariki akiwa na miaka 88 imehudhuriwa na viongozi wa juu wa serikali ya kijeshi nchini Misri,miongoni mwa viongozi wengine mashuhuri.

Maelfu ya wananchi wa Misri walijitokeza katika kanisa la Mtakatifu Mariko mjini Cairo kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo aliyewaongaza maelfu ya waumini wa dhehebu hilo tangu mwaka 1971.

Siku ya Jumanne nchini Misri ni siku ya kitaifa ya kuomboleza kifo cha askofu Senuda wa tatu aliyewaongoza zaidi ya waumini Milioni 10 wa dhehebu hilo la Coptic.

Bendera nchini humo zimepepea nusu mlingoti na usalama umeimarishwa katika mkoa wa Beheira anakozikwa.

Senuda atakumbwa kuwa kiongozi mtulivu na mhimiza amani na ambaye pia alikuwa karibuni na serikali ya Hosni Mubarak na wakosoaji wake wanasema hakuwatetea vema waumini wa Coptic walipovamiwa na kubaguliwa.

Kifo cha kiongozi huyo kimetokea wakati Misri ikiwa katika hali ya msukosuko wa kisiasa kutokana na mapinduzi yaliyofanyika nchini humo mwaka uliopita na kumwondoa kiongozi wa zamani Hosni Mubarak.

Askofu mkuu mpya atachaguliwa na viongozi wa kanisa hilo baada ya miezi kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.