Pata taarifa kuu
Nigeria

Watu kumi wauawa kwa shambulio la kujitoa Muhanga katika Kanisa moja nchini Nigeria

Shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lililotekelezwa nchini Nigeria katika Kanisa la Katoliki limesababisha vifo vya watu saba kitu ambacho kilichangia kuzuka kwa ghasia na polisi wakafyatua risasi na kuwaua watu wengine watatu.Β 

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amelaani vikali shambulizi hilo la bomu la kujitoa mhanga lililotekelezwa wakati wa ibada ya jumapili na kuwaacha watu kadhaa wakijeruhiwa kwenye tukio hilo baya.

Shambulizi hili linakuja ikiwa ni majuma mawili baada ya Kundi la Boko Haram kushambulia kanisa moja katika Jiji la Jos lakini hadi sasa hakuna kundi lolote ambalo limethibitisha kutekeleza shambulizi hili.

Katika hatua nyingine, waumini wa kikristo watatu wameuawa na watu wenye silaha karibu na katikati ya mji wa Jos, saa kadhaa baada ya watu kumi kuuawa katika tukio la shambulio la bomu la kujitoa muhanga katika kanisa la Katoliki.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.