Pata taarifa kuu
MISRI-CAIRO

Kesi dhidi ya wanaharakati nchini Misri yaahirishwa hadi April 10

Kesi inayowakabili wanaharakati wa demokrasia nchini Misri ambayo awali iliahirishwa kusikilizwa imeanza tena kusikilizwa hii leo kwenye mahakama kuu ya nchi hiyo. 

Moja ya maandamano ya amani nchini Misri kushinikiza kuachiwa huru kwa wanaharakati wanaoshikiliwa polisi
Moja ya maandamano ya amani nchini Misri kushinikiza kuachiwa huru kwa wanaharakati wanaoshikiliwa polisi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo awali iliahirishwa kusikilizwa kutokana na kujitoa kwa mmoja wa majaji wanaosikiliza kesi hiyo na kulazimika kuundwa kwa jopo jingine la majaji wapya ambao watasikiliza kesi hiyo.

Kesi hiyo ambayo inawahusu wanaharakati 43 ambao kati yao 16 ni raia wa Misri wakati 27 ni raia wa kigeni ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya kujipatia fedha kinyume cha sheria na kuendesha harakati zilizotishia usalama wa taifa.

Hivi karibuni Serikali ya nchi hiyo ilitangaza kuondoa marufuku ya kusafiri nje ya nchi hiyo kwa watuhumi wa kigeni ambao walikuwa wamejumuishwa kwenye kesi hiyo.

Miongoni mwa raia wa kigeni wapo raia kumi na tisa wa Marekani ambao wanadai kukamatwa kwao kumechochewa kisiasa na kwamba taasisi zao zilianzishwa kihalali kwa malengo ya kusaidia jamii.

Kufunguliwa mashtaka kwa raia hao kulifanya hata uhusiano kati ya nchi hiyo na Marekani kuwa mashakani baada ya nchi hiyo kutishia kusitisha msaada wake kwa nchi hiyo endapo isipowafutia mashtaka raia wake.

Hata hivyo Serikali ya Misri imeendelea kushikilia msimamo wake wa kuendelea na kesi hiyo huku wizara ya mambo ya nje ya Marekani ikisema inapitia jalada la kesi hiyo kuangalia namna ya kuweza kuwasaidia raia wake.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo wamekuwa wakishinikiza serikali ya Misri kufuta kesi hizo yakisema kuwa kuwafungulia mashtaka wanaharakati hao kunalenga kudumaza demokrasia ya taasisi zisizo za kiserikali kufanya kazi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.