Pata taarifa kuu
SUDAN-SUDAN KUSINI

Uhusiano kati ya serikali ya Khartoom na Juba waendelea kuzorota kufuatia mgogoro wa mafuta

Mvutano kati ya serikali ya Sudan na Sudan kusini kuhusu mafuta umeendelea kuchukua sura moya baada ya serikali ya juba kusisitiza kuwa hatofungua bomba lake kuu la mafuta linalopitia mjini Khartoom. 

David Buom Choat, muwakilishi wa Sudan Kusini kwenye Umoja wa Mataifa akieleza kuhusu mgogoro kati ya nchi yake na Sudan
David Buom Choat, muwakilishi wa Sudan Kusini kwenye Umoja wa Mataifa akieleza kuhusu mgogoro kati ya nchi yake na Sudan Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umekuja kufuatia juma lililopita ndege za Sudan kufanya mashambulizi ya anga kwenye mji wa El Nar na kuharibu miundombinu ya mafuta jambo ambalo limeonekana kuikera serikali ya Juba.

Mgogoro huo unaendelea kushika kasi wakati ambapo hapo kesho ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuwa na mzungumzo na pande zinazokinzana mjini Addis Ababa Ethiopia kwa lengo la kujaribu kusuluhisha mgogoro huo.

Umoja wa Afrika mara kadhaa umekuwa ukijihusisha moja kwa moja na mgogoro wa Sudan ambapo umekuwa ukisisitiza pande hizo kuafikiana na kumaliza tofauti zao.

Serikali ya Khartoom imekanusha majeshi yake kuhusika na mashambulizi yoyote juma lililopita kwenye ardhi ya Sudan Kusini na kusema kuwa yenyewe haikushiriki kwenye mashambulizi ndani ya ardhi hiyo bali waikaboliana na waasi wa JEM.

Sudan Kusini ilijitenga na Sudan mwaka jana mwezi wa saba baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo kadhaa ambapo toka kujitenga kwake kumekuwa na mvutano wa maneno na serikali ya Khartoom na kuzua hofu ya kuzuka vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.