Pata taarifa kuu
SENEGAL-DAKAR

Tume ya uchaguzi nchini Senegal yatangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi wa duru la pili

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Senegal hatimaye imetangaza tarehe 25 ya mwezi wa tatu mwaka huu kuwa tarehe rasmi ya kufanyika kwa duru la pili la uchaguzi mkuu wa Urais kati ya mahasimu wawili Abdoulaye Wade na kiongozi mkuu wa upinzani Macky Sall. 

Wananchi wa Senegal wakipiga kura kwenye duru la kwanza, ambapo sasa tarehe 25 watapiga kura kwenye duru la pili
Wananchi wa Senegal wakipiga kura kwenye duru la kwanza, ambapo sasa tarehe 25 watapiga kura kwenye duru la pili Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo ambalo limetolewa hii leo, limewataja mahasimu hao kuwa ndio watakaoshiriki kwenye duru la pili la uchaguzi huo kutokana na uchaguzi wa awali kumalizika bila kumpata mshindi wa jumla.

Siku ya jumamosi rais Wade aliiagiza tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo kurejea kuhesabu kura za majimbo ya kusini mwa nchi hiyo kwa lengo la kupata ukweli wa kura ambazo zilipigwa kwenye maeneo hayo.

Tume hiyo inayo siku tano kuhakikisha inarejea kuhesabu kura za majimbo ya kusini mwa nchi hiyo baada ya kuwepo taarifa kuwa kuna wizi wa kura ulifanyika ili kuupa upinzani ushindi kwenye uchaguzi huo.

Lakini hata kama tume ya taifa ya uchaguzi ikarudia kuhesabu kura hizo na kupata matokeo tofauti hayataathiri duru la pili la uchaguzi wa urais nchini humo ambao sasa utashuhudia wananchi wakipiga kira tarehe 25 a mwezi huu.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa uchaguzi wa duru la pili utakuwa wa upinzani mkali kwa rais Wade mwenye umri wa miaka 85 ambaye amepingwa na upinzani kuwania urais kwa muhula wa tatu wakidai kuwa amekwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Kiongozi mkuu wa upinzani Macky Sall ambaye pia aliwahi kuwa waziri mkuu kwenye serikali ya rais Wade anapewa nafasi kubwa ya kuweza kuibuka mshindi kwenye uchaguzi huo licha ya kuwa rais Wade pia anayonafasi ya kurejea madarakani.

Rais Wade amekaa madarakani kwa miaka kumi na mbili ambapo sasa anataka kuwania nafasi hiyo kwa muhula wa tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.