Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ANC

Kamati kuu ya umoja wa vijana wa ANC yaunga mkono Julius Malema kukata rufaa

Kamati kuu ya Umoja wa Vijana wa chama tawala nchini Afrika kusini cha African Nationa Congress ANC iliyokutana hii leo jiji Johannesburg imesema kuwa kiongozi wao Julius Malema atakata rufaa dhidi ya huku ya kufukuzwa uanachama iliyotolewa na kamati ya nidhamu ya chama hicho. 

Kiongozi wa Umoja wa Vijana wa ANC Julius Malema ambaye amefutwa uanachama na kamati ya nidhamu
Kiongozi wa Umoja wa Vijana wa ANC Julius Malema ambaye amefutwa uanachama na kamati ya nidhamu Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umetangazwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho Ronald Lamola na kuongeza kuwa wao kama Umoja wa Vijana wa ANC wanamuunga mkono kiongozi wao na watamsaidia kwenye kukata rufaa.

Juma lililopita kamati ya nidhamu ya chama cha ANC ilitoa uamuzi wa kumfukuza kabisa uanachama wa ANC Julius Malema kwa kile ilichodai kuwa kiongozi huyo wa vijana amekuwa akipandikiza chuki miongoni mwa wanachama kwa lengo la kukigawa chama.

Umoja wa vijana kwenye taarifa yao wamesema kuwa kusimamishwa na baadae kufutwa uanachama kwa Malema kulitokana na msukumo wa kisiasa ndani ya chama hicho ambapo baadhi ya viongozi wa juu wanaogopa utashi wake wakisiasa.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa endapo Malema atawasilisha rufaa yake basi ataendelea kuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ANC mpaka pale rufaa yake itakaposikilizwa tena na kutolewa uamuzi.

Kamati ya umoja wa vijana ya ANC imeapa kutoendeshwa kisiasa na watu wachache ambao wanataka kuuvuruga umoja huo.

Mara baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo juma lililopita, Malema mwenyewe alisema hajakata tamaa na kwamba atapambana kupata haki yake ambayo amedai anataka kupokonywa na watu wachache.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.