Pata taarifa kuu
ERITREA

Mwanasiasa wa upinzani wa Eritrea ahofiwa kutekwa Sudan

Afisa wa chama cha upinzani cha PDP nchini Eritrea haonekani na hajulikani aliko katika eneo la Sudan Mashariki na kuna wasiwasi kwamba huenda ametekwa na maafisa usalama wa Asmara.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema kuwa afisa huyo wa upinzani Mohamed Ali Ibrahim alitoweka nyumbani kwake kwenye mji wa Kasala siku ya Jumanne na hajaonekana mpaka sasa.

Polisi wa Sudan na hospitali za mji wa Kassala hazijatoa taarifa yeyote kuhusu mwanasiasa huyo na umoja wa Mataifa umesema kuwa zaidi ya wananchi 2000 wa Eritrea huvuka mpaka na kuingia nchini Sudan hususa katika eneo la Mashariki kusaka makazi kila mwezi.

Wakati huohuo Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa tofauti zao juu ya kugombea maeneo yenye utajiri mkubwa wa mafuta na Sudan zimechangia kwa kiwango kikubwa kuharibu uhusiano wake na Taifa la China.

Mpatanishi Mkuu kutoka Juba Pagan Amum amesema uhusiano wao na China umeingia dosari baada ya Serikali ya Khartoum kwa kushirikiani na Beijing kutaka kupora maeneo yanayozalishwa mafuta ya taifa hilo.

Serikali ya Juba imeweka bayana japokuwa uhusiano wao na China ndiyo ulikuwa unaanza vizuri lakini umetiwa dosari na Sudan lakini pia kutekwa kwa wafanyakazi wake kunaweza kukwamisha uhusiano mwema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.