Pata taarifa kuu
SUDANI

UN yasema muda uliotengwa kuwarejesha raia Sudani Kusini hautoshi

Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi duniani IOM limesema kuwa muda wa mwisho uliotengwa na serikali ya Sudan kuhakikisha kuwa zaidi ya raia nusu milioni wa Sudan kusini wanahamishwa nchini humo ni mdogo na hawawezi kufanikisha kwa wakati.

UN Photo/Isaac Billy
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa shirika hilo, Jumbe Omary Jumbe amesema kuwa ni jambo la kufikirika iwapo serikali ya Sudan inadhani kuwahamisha watu hao wote katika kipindi ambacho wametangaza itakuwa rahisi.

Uamuzi wa kurejeshwa nyumbani kwa raia wa Sudan Kusini zaidi ya nusu milioni walioko Sudan ulikuja baada ya juma lililopita viongozi wa nchi hizo mbili kutiliana saini kutekeleza mpango huo.

Nchi hizo mbili bado ziko katika mvutano mkubwa hata baada ya Sudani Kusini kujipatia uhuru wake Julai 9, mwaka jana na kujitenga na Sudan Kaskazini harakati zilizofanywa kwa kipindi kirefu.

Jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika kutatua mgogoro baina ya nchi hizo mbili lakini mpaka sasa bado kuna maeneo yenye migogoro na vita yakiwemo maeneo ya Blue Nile, South Kordofan na Abyei.

Suala la mafuta limekuwa kichocheo kikubwa cha mgogoro baina ya pande hizo mbili mpaka kufikia hatua ya Sudan Kusini kuacha kupitishia mafuta yake nchini Sudani Karthoum.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.