Pata taarifa kuu
NIGERIA

sita wapoteza maisha katika mlipuko flashpoint Nigeria

Uongozi wa jeshi nchini Nigeria umethibitisha kutokea kwa vifo vya watu sita katika milipuko miwili ya mabomu nje ya jengo la forodha mjini maiduguri nchini Nigeria.

Moja ya mashambulizi ya Boko Haram nchini Nigeria
Moja ya mashambulizi ya Boko Haram nchini Nigeria Reuters/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi hilo huko maiduguri kanali Hassan Mohamed alisema kuwa bado lawama za shambulizi hilo zinaelekezwa kwa kundi la kislamu la boko haram huku akitaja watu wanne miongoni mwa watu sita waliopoteza maisha wanatuhumiwa kuwa wanachama wa Boko Haram.

Wakazi wa maiduguri walishuhudia milipuko hiyo na kusema kuwa ndani ya dakika mbili milipuko ilitokea na kushuhudia watu wakipoteza maisha jirani na jengo la biashara.

Nchi ya Nigeria imekabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ambapo zaidi ya watu mia mbili wanakadiliwa kupoteza maisha katika kipindi cha miezi miwili.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.