Pata taarifa kuu
Sudani

Silaha kutoka Nchini Urusi na China zadaiwa kuendelea kuchochea Machafuko nchini Sudani

Shirika linalotetea haki za Bindamu ulimwenguni la Amnesty International, limezishutumu nchi za Urusi na China kuendelea kuipa silaha serikali ya Sudani ambayo inatumia silaha hizo kwa kuwauwa raia wasiokuwa na hatia katika Miji ya Mashariki mwa Nchi hiyo.

Msemaji wa Majeshi ya Sudani, Sawarmi Khaled Saad
Msemaji wa Majeshi ya Sudani, Sawarmi Khaled Saad
Matangazo ya kibiashara

Katika Ripoti iliochapishwa Jana Shirika hilo limeomba usitishwaji wa kuizia silaha Sudani, huku likitaka uheshimswaji wa vikwazo dhidi ya silaha vilivyo wekwa na Umoja wa Mataifa UN viheshimishwe katika nchi nzima.

Ni miaka kumi sasa tangu eneo la Darfur likumbwe na mzozo baina ya waasi na serikali inayoungwa mkono na makundi ya wapiganaji wa kiarabu wa janjawide. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa UN machafuko hayo yamesababisha vifo vya watu takriban laki tatu, lakini serikali ya Karthoum yasema watu elfu kumi, huku kiasi ya watu milioni moja na laki nane wakiyatoroka Makazi yao.

Miaka mitano iliopita Amnesty International ilitoa Ripoti kama hiyo kuhusu silaha zitakazo China na Urusi zinazo uziwa serikali ya khartoum. Ripoti hii mpya imetolewa baada ya kuzuka tena machafuko baina ya wanajeshi wa serikali na Makundi ya waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.