Pata taarifa kuu
SUDAN-SUDAN KUSINI

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir aonya kuhusu uwezekano wa kutokea vita kati ya nchi yake na Sudan

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ameonya kuhusu uwezekano wa kuzuka kwa vita kati ya nchi yake na serikali ya Khartoom iwapo mgogoro wa eneo la mafuta kwenye jimbo la Abyei hautashughulikiwa.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir akizungumza na waandishi wa habari
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir akizungumza na waandishi wa habari UN Photo/Isaac Billy
Matangazo ya kibiashara

Rais Kiir ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari mjini Juba na kusema kuwa jambo hilo linatokana na vile ambavyo serikali ya Sudan Kaskazini imekuwa ikihujumu mafuta yanayopelekwa mjini Juba.

Kauli ya rais Kiir imekuja kufuatia hivi karibuni serikali ya Kahrtoom kupendekeza mpango mpya wa kugawana mafuta ambapo ilipendekeza nchi ya Sudani Kusini kuwa inalipa shilingi bilioni 5.4 kwa Khartoom na pia serikali hiyo kuchukua mapipa 35 elfu ya mafuta kama fidia.

Katika mkutano wake na waandhi wa habari rais Kiir amesema kuwa kamwe yeye wala nchi yake haiwezi kukubaliana na maazimio hayo kwakuwa hayalengi kutatua mgogoro wa mafuta uliopo badala yake unalenga kuchochea machafuko zaidi.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa kukubaliana na mapendekezo hayo ni kufanya usaliti kwa wananchi wake waliomchagua kwa kura nyingi na kwamba serikali yake itaendelea kutumia mfumo wa awali waliokubaliana na Sudana kugawana mafuta nusu kwa nusu.

Mwezi wa kwanza mwaka huu serikali ya Juba ilitangaza kufunga bomba lake kuu la mafuta linaloelekea Khartoom katika kuonyesha kuchukizwa kwake na serikali hiyo kuiibia mafuta mengi na kufanya maamuzi bila kuwashirikisha.

Umoja wa Mataifa pia umeonya kuhusu uwezekano wakutokea mapigano kati ya nchi hizo mbili ikiwa jumuiya ya kimataifa haitaingilia kati mapema kutatua mgogoro wa mafuta uliopo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.