Pata taarifa kuu
MISRI-CAIRO

Baraza la kijeshi nchini Misri latangaza siku 3 za maombolezo kufuatia vifo vya mashabiki wa mpira

Baraza la kijeshi nchini Misri limetangza siku tatu za maombolezo kufuatia vurugu kati ya mashabiki wa timu za al-Masry na al-Ahly ambapo mashabiki zaidi ya 74 wameripotiwa kuuwa katika vurugu hizo.

Mashabiki wa timu ya al-Masry na al-Ahly wakipigana mara baada ya mechi
Mashabiki wa timu ya al-Masry na al-Ahly wakipigana mara baada ya mechi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea katika mji wa Port Said ambapo kulikuwa na mechi ya ligi kuu kati ya mahasimu hao wawili ambapo mara baada ya mchezo huo kumalizika mashabiki wa pande zote mbili walianza kukabiliana kwa mawe na visu.

Vurugu hizo zilizuka baada ya kushuhudia timu ya al-Masry kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabo matatu kwa moja na hivyo kuwafanya mashabiki wa al-Ahly kuanzisha vurugu na baadae vurugu hizo kuwa mbaya zaidi kiasi cha polisi kushindwa kuzidhibiti.

Mara baada ya vurugu hizo kiongozi wa baraza la kijeshi Field Marshal Hussein Tantawi alitangaza siku tatu za maombolezo na kuahidi serikali yake kufanya uchunguzi kuhusiana na chanzo cha vurugu hizo.

Kumeripotiwa kupangwa kufanyika kwa maandamano na mashabiki wa al-Ahly kuelekea kwenye ofisi za wizara ya mambo ya ndani kupinga hatua ya jeshi la Polisi kushindwa kudhibiti vurugu hizo zilizopelekea kutokea kwa vifo vingi.

Mbali na serikali kutangaza kufanyia uchunguzi tukio hilo, pia chama cha soka kimesema kitawahoji viongozi wa timu zote mbili pamoja na kutazama adhabu ambazo timu hizo zinaweza kupewa kutokana na vurugu hizo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.