Pata taarifa kuu
DAKAR-SENEGAL

Upinzani watishia kufanya maandamano zaidi nchini Senegal

Upinzani nchini Senegal umeendelea kusisitiza kuitisha maandamano zaidi nchini humo kushinikiza rais Abdoulaye Wade kutowania muhula wa tatu wa urais.

Mmoja wa waandamanaji nchini Senegal akirusha jiwe kwa Polisi
Mmoja wa waandamanaji nchini Senegal akirusha jiwe kwa Polisi Reuters/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Hapo jana watu kadhaa wamejeruhiwa kufuatia makabiliano kati ya polisi na waandamanaji ambao wameendelea kuweka kambi mjini Dakar kupinga hatua ya mahakama kuu ya katiba nchini humo kumuidhinisha rais Wade kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Kufuatia maandamano hayo, katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ametoa wito kwa wanaharakati wa kisiasa na asasi za kiraia zinazounga mkono mabadiliko ya kidemokrasia nchini humo kuwa watulivu katika kipindi hiki.

Zaidi ya waandamanji elfu moja wameendelea kuweka kambi mjini Dakar kushinikiza rais Wade kutowania tena urais.

Serikali ya Marekani nayo imewataka wananchi kuwa na utulivu wakati huu nchi hiyo inapoelekea katika mabadiliko ya kidemokrasia na kuelezea kusikitishwa kwake na hatua hiyo ya rais Wade.

Ikulu hiyo imeongeza kuwa inaona kuwa kitendo cha rais Wade kuendelea kuwania urais wa nchi hiyo kutazorotesha hali ya usalama na kunyima uhuru wa demokrasia kitu ambach kitaharibu yale yote mazuri ambayo rais huyo ameyafanya.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.