Pata taarifa kuu
DAKAR-SENEGAL

Serikali ya Senegal yazuia maandamano ya upinzani yaliyopangwa kufanyika kuanzia leo

Wizara ya mambo ya ndani nchini Senegal imetangaza kupiga marufuku maandamano yliyoitishwa na vyama vya upinzani hii leo kupinga uamuzi wa Mahakama ya Katiba kumuidhinisha rais Abdoulaye Wade kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Wananchi wakiandamana nchini Senegal, maandamano haya yalikuwa ni yakumuunga mkono rais wade
Wananchi wakiandamana nchini Senegal, maandamano haya yalikuwa ni yakumuunga mkono rais wade AFP PHOTO / Seyllou
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa wizara hiyo, Abdoulaye Thiam amesema kuwa Serikali imepiga marufuku maandamano hayo kwasababu za kiusalama kutokana na maandamano ya awali kuwa na madhara.

Hii leo vyama vya upinzani nchini humo vilitangaza kuitisha maandamano ya nchi nzima kushinikiza Mahakama ya Katiba kubatilisha uamuzi wake na kumzuia rais wade kuwania muhula wa tatu wa urais.

Maandamano hayo pia yaliyoitishwa na upinzani yanalenga kupinga uamuzi mwingine wa Mahakama hiyo kutangaza kuwazuia wagombea wengine watatu kuwania urais akiwemo mwanamuziki mkonge Youssou Ndour kwa madai ya kushindwa kupata sahihi elfu kumi zinazotakiwa kisheria kumruhusu kuwania urais.

Maandamano hayo yaliungwa mkono na asasi zisizo za kiraia kuwaunga mkono wapinzani kupinga kuvunjwa kwa Katiba ya nchi hiyo na kumuidhinisha rais Wade kuwania urais.

Maandamano ya juma lililopita yalishuhudia polisi mmoja akipoteza maisha wakati wakituliza ghasia za waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.