Pata taarifa kuu
DAKAR-SENEGAL

Upinzani nchini Senegal waitisha maandamano zaidi hii leo

Upinzani nchini Senegal hii leo umeitisha maandamano makubwa ya nchi nzima kupinga uamuzi wa mahakama siku ya Ijumaa kumdhibitisha rais Abdoulaye Wade kuwa anaweza kuwania urais kwa muhula wa tatu. 

Wananchi wa Senegal wakiandamana siku ya Ijumaa baada ya kutolewa kwa uamuzi wa Baraza la Katiba
Wananchi wa Senegal wakiandamana siku ya Ijumaa baada ya kutolewa kwa uamuzi wa Baraza la Katiba REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo ya upinzani yameitishwa ikiwa tayari kumeshuhudiwa watu kadhaa wakipoteza maisha siku ya Ijumaa mara baada ya uamuzi wa mahakama kutangaza kuwa rais Wade anaruhusiwa kikatiba kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Upinzani nchini humo uliwasilisha pingamizi katika Baraza kuu la Katiba nchini humo kutaka kumzuia rais Wade asiwanie urais kwa muhula watatu kwa kile walichodai kuwa Katiba ya nchi hiyo haikuwa inamruhusu kufanya hivyo.

Baraza hilo mbali na kuamua kuwa rais Wade anaweza kuwania urais kwa muhula wa tatu, pia lilitupilia mbali madai ya rais Wade kutaka wagombea watatu waondolewe kwenye kinyang'anyiro hicho kwa kukosa sifa.

Upinzani nchini Senegal bado umeendelea kusisitiza kuwa Katiba ya nchi hiyo inamuruhusu rais kuwania kwa mihula miwili peke yake na sio kama rais Wade anavyotaka kugombea kwa muhula watatu.

Waandamanaji wameapa kutoondoka kwenye miji mbalimbali ya nchi hiyo kuendelea kupinga Uamuzi wa Baraza la Katiba.

Mwanamuziki Youssou Ndour mara baada ya kutangazwa kwa uamuzi huo aliwashurumu vikali majaji waliotoa maamuzi hayo akisema kuwa ni aibu kwa viongozi hao kununuliwa wazi na rais wade na kupindisha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.