Pata taarifa kuu
Nigeria

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan aahidi kupunguza gharama za mafuta, baada ya kutoafikiana na vyama vya Wafanyakazi

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza kupunguza makato ya bei ya mafuta ili kumaliza mgomo wa kitaifa ambao sasa uko kenye wiki ya pili.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan REUTERS/ Daniel Munoz
Matangazo ya kibiashara

Jonathan ametangaza hatua hiyo kupitia Televisheni ya Taifa baada ya wiki nzima kuwa kimya mpaka pale wafanyakazi walipokubaliana kusitisha uzalishaji wa mafuta na Gesi nchini humo.
 

Tangazo la Jonathan kuwa mafuta yatashushwa kwa kiasi cha asilimia thelathini limekuja baada ya mazungumzo kati yake na vyama vya wafanya kazi kugonga mwamba.
 

Vyama vya wafanyakazi vimeahidi kuendelea kuweka shinikizo kwa njia ya mgomo ingawa wametaka kusitishwa kwa maandamano ya mitaani kwa sababu za usalama, hata hivyo asasi za kiraia na makundi ya kisiasa yameitisha maandamano.
 

Serikali ya Nigeria ilisitisha ruzuku ya mafuta tarehe 1 mwezi huu, na kusababisha gharama za mafuta kupanda zaidi ya mara mbili na kusababisha kuzuka kwa mgomo na maandamano yaliyoanza tarehe 9 mwezi huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.